Itakuwaje iwapo ufunguo wangu haufanyi kazi?
Ukipokea ujumbe kuhusu hitilafu: “Inaonekana kuwa ufunguo wako si sahihi. Hali hii ikitokea tena, tafadhali wasiliana na msimamizi wako wa huduma.” Fuata hatua zilizo hapa chini ili utatue hitilafu:
- Hakikisha unaweka ufunguo kamili, ikiwa ni pamoja na herufi tano za kwanza, “ss://”, ambazo haziwezi kunakiliwa kiotomatiki kwenye ubao wa kunakili. Huu ni mfano wa jinsi ufunguo kamili unavyoonekana (sampuli pekee; hautafanya kazi):
ss://[email protected]:39485/?outline=1
- Iwapo ufunguo wako hauwezi kunakiliwa kwenye ubao wa kunakili kabisa, hii inaweza kutokana na mfumo au programu yako ya kutuma ujumbe. Hali hii inaweza kutokea unapopokea ujumbe kutoka kwa mtu ambaye hayupo katika orodha yako ya anwani. Iwapo unanakili msimbo kutoka kwenye ujumbe, hakikisha umemweka mtumaji kwenye anwani zako, kisha ujaribu tena kufikia kiungo.
- Iwapo umekamilisha hatua ya 1 na ya 2 na bado unapokea ujumbe kuhusu hitilafu, inawezekana kuwa seva imezuiwa au ufunguo si sahihi tena. Ikiwa wewe ni msimamizi wa huduma, jaribu kubuni ufunguo wako mpya. Vinginevyo, wasiliana na msimamizi wako wa huduma ili upate ufunguo mpya.