Kwa nini siwezi kufikia intaneti ijapokuwa nimeunganishwa kwenye seva ya Outline?
Ikiwa unatumia simu ya mkononi, jaribu kubadilisha kati ya data ya mtandao wa simu na miunganisho ya Wi-Fi. Wakati mwingine aina moja ya muunganisho hufanya kazi wakati nyingine haifanyi. Iwapo unatumia kompyuta, jaribu kutenganisha na mtandao wenye bendi pana kisha uunganishe tena.
Ukiendelea kukumbwa na matatizo, inawezekana kuna tatizo katika seva yako ya Outline. Wasiliana na msimamizi wako wa huduma ili upate ufunguo mpya wa seva mbadala. Anaweza pia kuongeza kikomo cha data chahttps://google-jigsaw--jigsawuat.sandbox.my.site.com/outline/s/article/Terminologyufunguo wako iwapo ufunguo umezidi kiwango chake kinachoruhusiwa.