Ninawezaje kuweka mipangilio ya seva ya Outline?
Hatua ya kwanza ya kutumia Outline ni kuweka mipangilio ya seva ya Outline. Ni lazima wewe au mtu unayemwamini aweke mipangilio ya seva ili uweze kuunganisha kwenye intaneti huria kupitia Outline.
Kabla ya kuanza
Kabla ya kuanza kuweka mipangilio ya seva ya Outline, utahitaji vitu vichache:
- Uwezo wa kufikia seva zako au mtoa huduma za Wingu, kama vile DigitalOcean, Amazon Web Services (AWS) au Mfumo wa Wingu la Google (GCP).
Ikiwa huna uwezo wa kufikia seva ya wingu papo hapo, unaweza kufungua akaunti kwa urahisi kupitia mtoa huduma yeyote, ikiwa ni pamoja na walioorodheshwa hapo juu. Huenda ukahitaji kadi ya mikopo ili ujisajili. 2. Kompyuta ya mezani inayotumia macOS 10.9 kwenda juu, Windows 7.0 kwenda juu au Linux. 3. Programu ya Kidhibiti cha Outline.
Kuweka mipangilio kupitia DigitalOcean
Tumerahisisha kwa yeyote mchakato wa kuweka Outline ukitumia DigitalOcean kwa hatua chache. Baada ya kupakua na kuweka Kidhibiti cha Outline kwenye kompyuta yako, unaweza kuteua chaguo la kuweka mipangilio ya DigitalOcean, litakalokuelekeza kwenye hatua chache rahisi katika skrini za kuweka mipangilio na kuweka Seva yako ya Outline kwenye kifaa.
Kuweka mipangilio kupitia mtoa huduma mwingine wa wingu
Baada ya kupakua na kuweka Kidhibiti cha Outline, unaweza kuchagua kuweka seva ya Outline kwenye mashine pepe ukitumia AWS, GCP, DigitalOcean au mtoa huduma mwingine. Kila mazingira ni tofauti, kwa hivyo tumejumuisha maagizo kwenye utaratibu wa kuweka mipangilio wa Kidhibiti cha Outline kwa watoa huduma za wingu wanaotumika sana, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuweka mipangilio katika mashine yako pepe kabla ya kutekeleza hati ya kuweka Outline kwenye seva.
Je, unahitaji usaidizi zaidi?
Angalia sehemu yetu ya Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kuweka mipangilio ya seva ya Outline.