Hitilafu za kinga mtandao
Kuna aina tatu za matatizo ya kinga mtandao ambayo huenda ukakumbana nayo:
Huenda ukazuiwa na mtandao uliokingwa.
Ikiwa unajaribu kuweka Outline ukiwa umeunganisha na mtandao uliokingwa, kama vile shuleni au mahali pako pa kazi, jaribu kuweka ukitumia mtandao tofauti.
Hatua hiyo isipofanya kazi, tafadhali wasiliana na msimamizi wa mtandao wako ili aruhusu miunganisho kati ya mtandao uliokingwa na seva yako ya Outline. Utahitaji kujua anwani ya IP ya seva yako ya Outline na milango ambako Outline inatekelezwa, ambayo imeonyeshwa mwishoni mwa hati ya uwekaji.
Huenda ukazuiwa na kinga mtandao ya kifaa.
Iwapo una programu katika kifaa chako inayozuia miunganisho inayotoka kwenye milango isiyo ya kawaida au programu isiyotambulika, (ZoneAlarm kutoka CheckPoint), tafadhali soma hati ya kifaa au ya programu yako ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuzuia Outline isiathiriwe.
Huenda ukazuiwa na kinga mtandao ya seva.
Huenda mtoa huduma za wingu uliyemchagua akahitaji uweke mwenyewe kanuni ambazo hungependa zifuatwe na kinga mtandao ya seva yako ili uweze kufungua milango ambako Outline inatekelezwa. Baada ya kutekeleza hati ya usakinishaji, ulipaswa kuonyeshwa milango miwili iliyochaguliwa kwa unasibu ambako Outline inatekelezwa kwenye seva yako. Kufungua milango hii miwili kunatosha.
Ili uweke kanuni ambazo hungependa zifuatwe na Kinga mtandao ya seva yako, tunapendekeza uangalie hati za 'ufw' na 'iptables':