Skip to main content

Jinsi Outline Inavyofanya Kazi

Kuweka seva kwenye kifaa

​Ingawa uwekaji wa Outline kwenye kifaa unaweza kuonekana rahisi, ukweli ni kuwa kuna mkusanyiko wa hatua changamano zinazoendelea chinichini ili uweke seva yako kwenye kifaa. Kila wakati Outline inapowekwa kwenye kifaa, hati ya uwekaji hutekeleza hatua zifuatazo:

  • Toleo thabiti la picha ya Shadowbox huletwa na kupakiwa kwa kutumia Docker. Picha hiyo hupangishwa kwenye Quay.io, katika https://quay.io/repository/outline/shadowbox?tab=tags. Picha hiyo ina seva ya Outline na Management API ambayo baadaye hutumiwa na programu ya Kudhibiti Seva ya Outline ili kuweka na kuondoa funguo, kuchagua au kutochagua kuripoti vipimo visivyokutambulisha, nk.
  • Watchtower huwekwa kwenye kifaa na kuwekewa mipangilio ili iangalie iwapo kuna masasisho ya picha kila saa. Hali hii huhakikisha kuwa kila seva ya Outline imesasishwa kila wakati kwa vipengele na maboresho mapya zaidi ya usalama.
  • Seva ya wavuti inayotumiwa kufikia Management API, huanzishwa kwenye mlango nasibu kwenye njia ya siri inayochaguliwa kwa unasibu.
  • Cheti cha SSL kinachojitia saini huundwa ili udhibiti wa seva ya Outline usimbwe kwa njia fiche kwa kutumia TLS licha ya kutokuwepo kwa jina la kikoa. Alama bainifu ya kipekee ya cheti hiki hubuniwa na kuhifadhiwa kwenye programu ya Kidhibiti cha Outline. Hali hii husaidia kuzuia mashambulizi ya MITM.

Outline ikishawekwa kwenye kifaa, haihitaji kuwekewa mipangilio yoyote.

Usalama wa seva

Outline ni programu huria, hivyo basi mtu yeyote anaweza kuona na kuboresha msimbo iwapo atagundua uwezekano wa kuathirika. Msimbo wetu hupangishwa kwenye GitHub.

Zaidi ya hayo, seva zote za Outline zilizowekwa husasishwa kiotomatiki wakati wowote toleo jipya linapochapishwa. Hali hii huhakikisha kuwa hakuna seva yoyote ya Outline inayotumia matoleo ya zamani ya programu.

Ili kudhibiti funguo kwenye seva, programu ya Kidhibiti cha Outline hushirikiana na Huduma ya Kudhibiti kwenye seva ya Outline. Huduma hiyo ya Kudhibiti hutekelezwa kwenye mlango nasibu na kwenye njia ya siri na ya kipekee inayochaguliwa kwa unasibu. Huduma ya Kudhibiti haiwezi kuchunguzwa kwa sababu haijibu hoja isipokuwa njia husika ya siri ibainishwe. Mwisho, mawasiliano yote yanayotumwa kwenye Huduma ya Kudhibiti husimbwa kwa njia fiche kwa kutumia cheti cha SSL kinachojitia saini.

Pia, seva ya Outline haihifadhi kumbukumbu zozote, kwa hivyo hata ikiathiriwa, hakuna data yoyote ya mtumiaji inayoweza kufumbuliwa. Pata maelezo zaidi hapa. Outline ilikaguliwa na Radically Open Security pamoja na Cure53 mwaka wa 2018. Angalia ripoti hizo hapa.

Kushughulikia shughuli za UDP

Outline inaweza kutumika kama VPN ya mfumo mzima, kumaanisha kuwa shughuli zote za UDP hupitishwa kwenye seva ya Outline.

Shughuli za DNS

Outline huleta rekodi zote za utafutaji wa DNS kupitia seva ya Outline na kuzilinda kwa kutumia usimbaji fiche ule ule unaotumika kwenye shughuli nyingine zote za mtandao. Hoja zako za DNS zitapitia kwenye seva ya Outline na kutumwa kwenye Dyn Internet Guide, OpenDNS, Cloudflare DNS au Quad9 DNS. Outline kamwe haihifadhi kumbukumbu za rekodi zako za kutafuta DNS.