Skip to main content

Kwa nini siwezi kuweka programu ya Outline kwenye Windows?

Unaweza kuona ujumbe huu kuhusu hitilafu: “Samahani, inaonekana kuwa programu ya Outline haijawekwa ipasavyo. Tafadhali jaribu kuiweka tena. Hatua hiyo isipotatua hitilafu, tafadhali tuma maoni.”

Ikiwa unatumia Outline kwenye Windows, wakati mwingine, huenda ukakumbwa na hitilafu isiyotarajiwa. Katika hali nyingi, unahitaji kufuta adapta ya TAP ya Outline (kiendeshaji) na uweke Outline upya.

Hatua zinaweza kutofautiana kulingana na toleo lako la mfumo wa uendeshaji wa Windows, lakini zifuatazo ni hatua za jumla za jinsi ya kuondoa adapta ya TAP na programu ya Outline kisha uweke upya programu ya Outline.

  1. Ondoa adapta ya TAP ya Programu ya Outline
    • Nenda kwenye Vidhibiti vya Vifaa, kisha Adapta za Mtandao
    • Tafuta faili ya “TAP-Windows Adapter V9 au adapta ya TAP inayohusishwa na Outline
    • Ondoa au ufute adapta hii. Kumbuka kuwa hatua hii inaweza kuathiri programu nyingine za VPN ambazo umeweka.
  2. Ondoa Programu ya Outline
    • Nenda kwenye Programu na Vipengele, kisha kwenye Ondoa Programu
    • Tafuta Programu ya Outline kisha uiondoe
    • Pakua toleo jipya kabisa la Programu ya Outline kisha uiweke upya kwenye kifaa chako cha Windows. Toleo hilo jipya la programu unaloweka linapaswa kuweka adapta mpya ya TAP kiotomatiki.

Iwapo bado unakumbwa na hitilafu, wasiliana na timu ya usaidizi.