Skip to main content

Jinsi ya kutuma maoni au mapendekezo

Asante kwa kusaidia kuboresha Outline! Kuna njia kadhaa za kututumia maoni, bila kujitambulisha au kwa kujumuisha anwani yako ya barua pepe ikiwa unahitaji jibu:

  • Kwa wasanidi programu: Outline ni programu huria na tunapangisha misimbo yetu yote kwenye GitHub. Unaweza kuchangia hoja zako kwenye GitHub au katika jumuiya yetu ya Reddit.
  • Kwa watumiaji: Unaweza kututumia maoni kupitia programu ya Outline au Kidhibiti cha Outline. Tueleze maoni yako yanahusu nini na ukipenda, tupe anwani yako ya barua pepe ili tuweze kukupa jibu kuhusu maoni hayo. Tunakusanya pia baadhi ya metadata kuhusu mazingira yako, ili tuweze kukusaidia kufanya uatatuzi, kama vile kivinjari chako, mfumo wa uendeshaji na toleo la programu unalotumia.
  • Kupitia tovuti hii: Unaweza kubofya kiungo cha 'wasiliana nasi' popote utakapokiona kwenye tovuti hii.
  • Matatizo makubwa: Ikiwa ungependa kuripoti tatizo kubwa la usalama, tungependa ututumie barua pepe yenye maelezo zaidi kupitia security [at] getoutline.org.

Asante tena kwa kuchukua muda wa kutupatia mawazo yako.