Kwa nini ninashindwa kuweka Kidhibiti cha Outline kwenye Windows?
Unaweza kuona ujumbe huu kuhusu hitilafu: “Samahani, inaonekana kuwa programu ya Outline haijawekwa ipasavyo. Tafadhali jaribu kuisakinisha tena. Ikiwa haitafanya kazi, tafadhali tuma maoni.”
Ikiwa unatumia Outline kwenye Windows, wakati mwingine, huenda ukakumbwa na hitilafu isiyotarajiwa. Katika hali nyingi, unahitaji kufuta adapta ya TAP ya Outline (kiendeshaji) kisha uweke Outline upya.
Huenda hatua zikatofautiana kulingana na toleo lako la mfumo wa uendeshaji wa Windows, lakini zilizo hapa chini ni hatua za jumla za jinsi ya kuondoa adapta ya TAP na Kidhibiti cha Outline kisha kuweka upya Kidhibiti cha Outline.
- Kuondoa adapta ya TAP ya Kidhibiti cha Outline
- Nenda kwenye Vidhibiti vya Vifaa, kisha Adapta za Mitandao
- Tafuta faili ya “TAP-Windows Adapter V9” au adapta ya TAP inayohusishwa na Outline
- Ondoa au ufute adapta hii. Kumbuka kuwa hatua hii inaweza kuathiri programu nyingine ulizoweka za VPN.
- Kuondoa Kidhibiti cha Outline
- Nenda kwenye Programu na Vipengele, kisha katika Ondoa Programu
- Tafuta programu ya Kidhibiti cha Outline kisha uiondoe
- Pakua toleo jipya kabisa la Kidhibiti cha Outline kisha uliweke upya kwenye kifaa chako cha Windows. Toleo hilo jipya la programu unaloweka linapaswa kuweka kwenye kifaa adapta mpya ya TAP kiotomatiki.
Iwapo bado unakumbwa na hitilafu, wasiliana na timu ya usaidizi.