Kudhibiti ufikiaji wa seva ya Outline (kwa kutumia funguo)
Ukishamaliza kuweka seva ya Outline, unaweza kuanza kuituma na kudhibiti uwezo wa watu wa kuifikia. Watu watakaopokea mwaliko kutoka kwako wataweza kupakua programu ya Outline ili waitumie kulinda shughuli yao kwenye intaneti.
Ruhusu ufikiaji wa seva yako ya Outline
Baada ya kuweka seva ya Outline, utaelekezwa kwenye ukurasa wa maelezo ya seva katika Kidhibiti cha Outline, ambapo unaweza kuunda funguo. Pata maelezo zaidi kuhusu funguo.
- Kuunda funguo: Bofya aikoni ndogo ya "+" katika sehemu ya chini ya ukurasa ili uunde funguo.
- Kutuma funguo: Katika upande wa kulia wa kila ufunguo, kuna aikoni ya kutuma unayoweza kubofya ili upate mwaliko. Nakili na ubandike mwaliko huu kwenye mfumo utakao wa kutuma na kupokea ujumbe.
Ombi la kipengele: Kuruhusu idhini ya kufikia kutoka kwenye programu ya Kidhibiti cha Outline
Wasimamizi wengi wa seva hutuomba turahisishe mchakato wa kutuma mialiko kwa kuwapa chaguo la kuweka anwani ya barua pepe ya mtu fulani moja kwa moja kwenye Kidhibiti cha Outline.
Tunasikitika kuwa huenda tusijumuishe kipengele hiki kwenye Kidhibiti cha Outline. Mojawapo ya kanuni zetu kuu ni kuimarisha faragha na usalama wa watumiaji wetu, kumaanisha kuwa hatukubuni sehemu yoyote ya kuweka anwani za barua pepe au maelezo ya mawasiliano.
Kwa sababu hii, tunawaomba wasimamizi wa seva watumie mfumo salama wa kutuma na kupokea ujumbe, kama vile barua pepe au gumzo salama, kutuma mwaliko kwa mtumiaji wa hatima.
Hatua atakazofuata mtumiaji baada ya kumtumia funguo
- Mtumiaji atabofya kiungo cha uwekaji kwenye kifaa chake
- Atapata kidokezo cha kusakinisha programu ya Outline ikiwa hajaisakinisha tayari
- Ataunganisha kwa mara ya kwanza kwenye seva yako ya Outline kupitia ufunguo wa kipekee uliopachikwa kwenye mwaliko
- Sasa anaweza kutumia kitufe cha unganisha au tenganisha ili adhibiti ufikiaji wake wa intaneti kupitia seva yako ya Outline
Kuondoa ufikiaji wa seva yako ya Outline
Kwenye ukurasa wa maelezo ya seva katika Kidhibiti cha Outline, upande wa kulia wa kila ufunguo kwenye seva, utaona menyu yenye chaguo la kufuta ufunguo. Kufuta ufunguo huondoa idhini ya mtumiaji ya kufikia seva yako.