Ukusanyaji wa Data na Taarifa
Outline haikusanyi taarifa binafsi isipokuwa ukichagua kuzitoa. Outline pia haikusanyi maelezo kuhusu tovuti unazotembelea au watu unaowasiliana nao wala mambo mnayowasiliana kuhusu.
Ikiwa unafungua au kuingia katika akaunti ukitumia mtoa huduma mwingine za wingu kupitia Kidhibiti cha Outline, hatupati taarifa zozote unazotoa kwa mtoa huduma wako mwingine za wingu, kama vile anwani ya barua pepe, jina, maelezo ya kulipa na maelezo yako ya malipo.
Maelezo tunayopata kiotomatiki
Sisi hukusanya aina mbili ya maelezo kiotomatiki.
- IP ya seva
IP ya seva ya Outline hukusanywa na Quay.io na kuonyeshwa kwetu wakati seva inasasishwa kiotomatiki kwa vipengele na usalama wa hivi karibuni ulioboreshwa. Huenda IP ya Seva ikatambua mtoa huduma za seva ya wingu na mji ambapo mipangilio ya seva ya Outline imewekwa, lakini hali hii haitoi maelezo kuhusu anayetekeleza seva au anayeifikia.
- Taarifa za kiufundi zisizomtambulisha mtu binafsi
Outline ikiacha kufanya kazi au hitilafu isiyofuata kanuni ikitokea au ukituma maoni wewe mwenyewe kupitia programu ya Outline, taarifa zilizoorodheshwa hapa chini zitaripotiwa. Taarifa hizi zitatumiwa tu kusaidia kutambua na kurekebisha matatizo ya uthabiti na utendaji.
- Nchi
- Lugha
- Tarehe na wakati wa kuacha kufanya kazi / hitilafu na hadi matukio 100 ya awali, kama vile mtumiaji anapofungua sehemu ya ‘Kuhusu’
- Arifa za hitilafu zilizokusanywa kwa njia tuli
- Jina na toleo la mfumo wa uendeshaji
- Muundo wa simu (panapohitajika)
- Muda unaotumika kufungua programu
- Kivinjari
- Usanifu programu
- Toleo na nambari ya muundo ya Outline
Taarifa hizi hutumwa kupitia HTTPS kwa Sentry (sentry.io), mtoa huduma mwingine wa kufuatilia hitilafu za programu huria. Sentry hutumia teknolojia na huduma mbalimbali za kiwango cha sekta ili kulinda data yako kutokana na kufumbuliwa, kutumiwa, kupotezwa na kufikiwa bila idhini. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera za Sentry, tafadhali tembelea https://sentry.io/security/ na https://sentry.io/privacy/ au uwasiliane na [email protected]. Data yote ya Outline iliyohifadhiwa na Sentry imezuiwa hivi kwamba ni washiriki tu wa timu ya Outline wanaoweza kuifikia.
Maelezo tunayopata tu unapojijumuisha
Outline huripoti taarifa zifuatazo kwa timu ya Outline unapojijumisha.
- Vipimo vya matumizi
Kila seva ya Outline hukusanya kiotomatiki, kwa saa moja iliyopita na kulingana na matumizi ya kila ufunguo, idadi ya baiti iliyotumwa, muda ambao mtumiaji alikuwa ameunganishwa kwenye seva, mifumo huru na nchi ambako vitambulisho hivyo vimetumiwa na iwapo vipengele vyovyote vimewashwa au kuzimwa. Kumbukumbu za maudhui ya mawasiliano wala metadata inayomtambulisha mtu binafsi (k.m. vitambulisho vya kuingia katika akaunti, anwani za barua pepe, vitambulisho vya kifaa, nk) hazihifadhiwi. Vipimo vyote huhusishwa na kitambulisho cha seva. Unaweza kupata maagizo ya jinsi ya kubadilisha kitambulisho cha seva hapa.
Kwa chaguomsingi, Seva za Outline hazitumi vipimo hivi kwa timu ya Outline. Msimamizi wa Seva akichagua kwa namna wazi kutuma vipimo vya utumiaji, maelezo haya yatatumwa kwa timu ya Outline kwa njia salama kila saa. Baada ya siku 60, vipimo vya utumiaji vitajumlishwa katika kiwango cha nchi. Wasimamizi wa seva wanaweza kubadilisha mapendeleo yao ya kutuma vipimo vya utumiaji wakati wowote kwa kutembelea menyu ya ‘Mipangilio’ katika Kidhibiti cha Outline.
Tunakushukuru kwa kututumia vipimo visivyokutambulisha kuhusu matumizi yako ya seva, kwa kuwa tunavitumia kupima mitindo ya utumiaji na kuboresha bidhaa.
Kwa mfano, msimamizi wa Seva akichagua kututumia vipimo vya utumiaji, tunaweza kupokea maelezo kwamba Seva yenye kitambulisho cha 12345 ilitumiwa kwa saa 3 jana, ikatuma zaidi ya megabaiti 500 za data kutoka kwenye funguo tatu, kila ufunguo ukiwa umetumiwa nchini Marekani na Canada, ikiwa kipengele cha vikomo vya data kimewashwa.
- Maoni yako na anwani ya barua pepe unayotumia kuyatuma
Programu za Outline na Kidhibiti cha Outline hukuruhusu kuitumia timu maoni. Tunapendekeza kuwa usijumuishe maelezo yanayoweza kukutambulisha, lakini kuna sehemu ya barua pepe ambayo unaweza kujaza kwa hiari ikiwa ungependa kupokea jibu kutoka kwa timu. Sisi pia hukusanya maelezo fulani ya msingi moja kwa moja, ili tuweze kuelewa maoni yako. Tafadhali angalia kipengee cha 2 hapo juu, kwenye sehemu ya “Taarifa tunazopata kiotomatiki”, ili uone data tunayokusanya. Pata maelezo zaidi kuhusu desturi za Outline za faragha na usalama hapa.
Ikiwa unatumia toleo la beta la programu ya Outline kwenye Android, huenda tukatumia huduma ya Firebase kutoka Google kukusanya maelezo ya utatuzi yanayoweza kutusaidia kutambua matatizo na kuboresha Outline Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu sera za faragha na usalama za Firebase kwenye tovuti yao: firebase.google.com/support/privacy. Ikiwa hutaki Outline itume maelezo haya kupitia Firebase, tafadhali tumia toleo la umma la programu.