Mimi ni msanidi programu. Je, ninaweza kupata wapi usaidizi wa kujumuisha Outline SDK kwenye programu yangu?
Tovuti hii ya usaidizi ni ya watumiaji wa Programu na Kidhibiti cha Outline. Kwa wasanidi programu, tafadhali tumia GitHub ili upate usaidizi. Ili uulize swali, tafadhali chapisha kwenye Mfumo wa majadiliano wa SDK. Sehemu ya Mfumo wa majadiliano ni sehemu muhimu ya kuuliza maswali, kueleza mawazo, kupata viungo vya matoleo ya kujaribu na kuwasaidia wasanidi programu wengine kupitia Outline SDK. Ili utume maombi ya kupata vipengele au ripoti za hitilafu, tafadhali fungua Tatizo badala yake.