Istilahi
Je, VPN ni nini?
Mtandao pepe wa faragha (VPN) ni muunganisho wa faragha kati ya vifaa vyako na seva pangishi. Unapotumia VPN, shughuli zako kwenye intanet zinafichwa zisionekane kwa mtoa huduma wa intaneti. Huenda ukahitaji kutumia VPN katika hali zifuatazo:
- Kulinda data yako unapotumia Mtandao wa Wi-Fi ya umma
- Kuifanya data yako ya kuvinjari iwe ya faragha ili isionekane kwa mtoa huduma za intaneti na mashirika ya serikali
- Kufikia maudhui ambayo hayajadhibitiwa kutoka vyanzo mbalimbali duniani kote
Je, Outline inatofautiana kwa namna gani na VPN za kawaida?
Watoa huduma za intaneti wanaweza kutambua kwa urahisi na kuzuia VPN za kawaida kwa kubaini itifaki za kawaida za usalama na/au ishara za kiasi cha shughuli. Outline ni thabiti zaidi kuliko VPN za kawaida kwa sababu imeundwa kwa kutumia itifaki ambayo imebuniwa isiwe rahisi kutambuliwa na hivyo kuwa vigumu kuizuia. Outline haiwezi kuzuiwa kwenye miundo changamano ya uzuiaji ikiwa ni pamoja na uzuiaji kwenye mtandao na uzuiaji wa IP.
Je, seva ya Outline ni nini?
Seva ya Outline hutekeleza VPN ambayo watumiaji walioruhusiwa wataunganishwa nayo. Ikiwa unaanzisha mtandao mpya, unaweza kutumia seva iliyo salama kama seva yako ya Outline iwapo unayo au unaweza kutumia mtoa huduma za wingu kama vile:
- DigitalOcean
- Mfumo wa Wingu la Google (GCP)
- Amazon Web Services (AWS)
Utaweka mipangilio ya seva yako kwenye Kidhibiti cha Outline.
Je, msimamizi wa huduma ni nani?
Msimamizi wa huduma ni mtu anayewajibika kuweka mipangilio ya seva ya Outline na kutuma funguo kwa watumiaji. Kwa ujumla msimamizi wa huduma anawajibikia gharama za matumizi ya seva.
Je, ufunguo ni nini?
Ufunguo unatumika kufikia seva iliyopo ya Outline na kuunganisha kwenye VPN. Msimamizi wa huduma atakupatia ufunguo au unawezakuweka mipangilio ya seva ya Outline mwenyewe. Huu ni mfano wa jinsi ufunguo unavyoonekana (sampuli pekee; hautafanya kazi):
ss://[email protected]:39485/?outline=1
Kidhibiti cha Outline ni nini?
Kidhibiti cha Outline ni programu ya kompyuta ya mezani inayomwezesha msimamizi wa huduma kuweka mipangilio ya seva ya Outline, kubuni ufunguo na kuweka vikomo vya data katika matumizi kwa kila ufunguo. Unaweza kupakua toleo jipya kabisa la Kidhibiti cha Outlinehapa auhapa.
Programu ya Outline ni nini? Programu ya Outline ni programu, inayopatikana kwenye kompyuta ya mezani na simu, inayokuwezesha kuunganisha kwenye seva ya Outline na kufikia VPN ukitumia ufunguo. Unaweza kupakua toleo jipya kabisa la Programu ya Outlinehapa auhapa.
Je, vikomo vya data ni nini?
Kidhibiti cha Outline huwawezesha wasimamizi wa huduma kuweka kikomo cha data cha siku 30 zinazotangulia cha matumizi ya funguo ili kuzuia matumizi kupita kiasi na kusaidia kutabiri gharama zako. Wasimamizi wa huduma wanaweza kuweka kikomo chaguomsingi kinachotumika kwenye kila ufunguo na kuweka kikomo tofauti kwenye ufunguo wowote ili kubatilisha kikomo chaguomsingi. Baada ya kikomo kuwekwa, kikomo hicho huanza kutumika papo hapo na hutekelezwa kila saa.
Ikiwa wasimamizi wa huduma watachagua kuruhusu Jigsaw ifikie vipimo, wanapaswa kuangaliasera ya ukusanyaji data ili wapate maelezo kuhusu jinsi matumizi ya vikomo vya data yatakavyoripotiwa.