Skip to main content

Usalama na faragha unapotumia Outline

Usalama na faragha unapotumia Outline

Jinsi Outline inavyolinda mawasiliano yako mtandaoni

Shughuli kwenye intaneti huwa katika hatari zaidi ya kufuatiliwa zinaposafirishwa kupitia mtandao wa mahali ulipo au wa taifa lako.

Outline husaidia kuhakikisha kuwa mawasiliano yako ni ya faragha kwa kusimba kwa njia fiche shughuli zako kwenye intaneti inaposafiri ndani ya mtandao wa taifa lako na kuziweka katika hali hiyo hadi inapofikia seva ya Outline. Shughuli zinaposimbwa kwa njia fiche kwa kutumia Outline, wapelelezi wa mitandao hawawezi kukagua tovuti unazotembelea wala taarifa unazotuma.

Huenda Outline pia ikakusaidia kurejesha uwezo wa kufikia nyenzo salama za mawasiliano zilizosimbwa kwa njia fiche kuanzia mwanzo hadi mwisho ambazo huenda usiweze kuzifikia vinginevyo katika nchi uliko.

Viwango vya usimbaji fiche

Outline husimba kwa njia fiche mawasiliano kati ya kifaa chako na Seva ya Outline kwa kutumia msimbo wa AEAD 256-bit Chacha2020 IETF Poly 1305. Misimbo ya AEAD hukupa usiri, uadilifu na uhalisi na huonyesha utendaji bora zaidi kwenye maunzi ya kisasa.

Ukaguzi wa usalama

Mwaka 2018, Outline ilikaguliwa na Radically Open Security na Cure53, mashirika mawili huru ya usalama dijitali yanayokagua programu kulingana na viwango vipya vya usalama. Radically Open Security ilifanya ukaguzi wa ziada mwaka 2022 na Cure53 ilifanya ukaguzi wa Outline SDK mwaka 2024. Unaweza kusoma ripoti hapa:

Vipimo na kumbukumbu zinazoficha utambulisho wa data

Outline hufuatilia kipimo data kilichotumika, kama "baiti zilizotumwa" kwa kila ufunguo. Maelezo haya huwaruhusu wasimamizi wa seva kurekebisha inavyohitajika usajili wao wa kipimo data kwenye watoa huduma za seva za wingu wanazozitumia, lakini hayawaruhusu kuona taarifa halisi zilizopitia kwenye seva ya Outline.

Pata maelezo zaidi kuhusu ukusanyaji wa data na taarifa kwenye Outline.


Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu usalama na faragha

Je, Outline inaweza kuficha utambulisho wangu mtandaoni?

Hapana, Outline si zana ya kuficha utambulisho. Outline hulinda faragha yako dhidi ya wapelelezi wanaoweza kufuatilia mtandao.

Outline haifichi kikamilifu utambulisho wako kwenye tovuti unazotembelea, kwa sababu bado zinaweza kukutambulisha ukiingia katika akaunti na wakati mwingine kupitia mbinu kama vile ufuatiliaji wa alama bainifu kwenye kivinjari. Kwenye programu za vifaa vya mkononi, simu nyingi mahiri za kisasa zina API zinazoruhusu programu zilizosakinishwa kupata maelezo ya mahali ulipo bila kutegemea seva yako mbadala kwa sababu zinaweza kutegemea GPS iliyopachikwa.

VPN kwa jumla hutoa ulinzi muhimu, haswa dhidi ya ufuatiliaji kwenye intaneti, lakini bado kuna hatari fulani unapokuwa mtandaoni. Hata ukiwa na VPN, iwapo tayari Mtoa Huduma za Intaneti anafahamu utambulisho wako na anaweza kutazama trafiki ya mtandao wako, huenda akaweza kubaini anwani ya IP ya seva yako ya Outline. Taarifa hizi zinaweza kutumiwa kukuzuia usifikie seva ya Outline au kujifunza jinsi unavyotumia mtandao, kama vile wakati wa kawaida unapokuwa mtandaoni na ikiwezekana eneo la jumla uliko.

Mtu anaweza kujua kama ninatumia Outline?

Inawezekana. Mifumo na huduma unazofikia zinaweza kujua kuwa muunganisho wako unatoka kwenye seva ya wingu. Mara kwa mara, zinaweza kubaini kuwa unatumia VPN, lakini hazitaweza kuona yaliyomo katika shughuli zako kwenye intaneti.

Outline itanilinda kutokana na hatari zote zinazoweza kutokea za mashambulizi ya mtandaoni?

Hapana. Hakuna zana inayoweza kukulinda dhidi ya hatari zote zinazoweza kutokea za mashambulizi ya mtandaoni. Outline hukupa uwezo wa kufikia mtandao wazi na huimarisha faragha yako kwa kusimba trafiki yako kwa njia fiche, lakini tunapendekeza uchukue hatua za ziada za tahadhari ili ujilinde dhidi ya aina nyingine za mashambulizi, kama vile programu hasidi na wizi wa data binafsi.

Ili uimarishe ulinzi wako mtandaoni, tafadhali shirikiana na mtaalamu wa usalama wa mtandaoni wa shirika lako. La sivyo, unaweza kupata ushauri unaokufaa kutoka kwa wataalamu wa usalama wanaoongoza katika Security Planner, tovuti iliyobuniwa ili kukupa maagizo bayana kuhusu jinsi ya kuchagua nyenzo za usalama wa mtandaoni zinazokufaa.

Unaweza pia kuangalia bidhaa nyingine za usalama wa mtandaoni kutoka Jigsaw, kama vile Intra, Project Shield na Kilinda Nenosiri.

Je, ni halali kisheria kutumia VPN?

Tafadhali angalia sheria za mahali ulipo, kanuni na Sheria na Masharti ya huduma ya seva ya wingu unayopanga kutumia kabla ya kuendesha Outline au kutumia programu.