Skip to main content

Ninawezaje kupata ufunguo?

Outline si kama huduma za VPN unazolipia ili uzitumie; ni zana inayokuwezesha kutekeleza na kuruhusu ufikiaji wa seva ya VPN ya faragha. Msimamizi wa huduma ni mtu pekee anayeweza kutoa ufunguo. Timu ya Outline haisambazi funguo zinazolipiwa au zisizolipiwa. Hatuna washirika wowote rasmi wa ufunguo wa Outline, isipokuwa Paskoocheh katika Kifarsi.

Zifuatazo ni chaguo tatu za kupata ufunguo:

  • Mwombe mtu akualike kwenye seva yake: Ikiwa unamfahamu mtu aliye na seva ya Outline, wasiliana naye na umwombe akupe ufunguo.
  • Kuunda seva mwenyewe: Kwa kutumia kompyuta ya Windows, Mac au Linux, pakua Kidhibiti cha Outline kisha uweke seva yako ya Outline ya faragha. Tumerahisisha mchakato huu kwa mtu yeyote, hasa kupitia mtoa huduma wa seva ya wingu ya DigitalOcean.
  • Kutumia huduma ya Outline au Shadowsocks: Programu ya Outline pia inaweza kutumiwa pamoja na huduma za wengine zinazotumia itifaki ya Outline au Shadowsocks. Kwa mfano:
    • nthLink hutumia huduma isiyolipiwa inayotegemea Outline na toleo lililoboreshwa la programu ya Outline.
    • ASL19 hutumia toleo la Outline lililoboreshwa linaloitwa BeePass pamoja na kijibu cha Telegram kinachotoa funguo bila malipo kwenye seva za BeePass.
    • Watumiaji wanaozungumza Kifarsi wanaweza pia kuomba ufunguo wa Outline kutoka Paskoocheh ya ASL19.

Baada ya kupakua programu ya Outline, nakili kisha ubandike ufunguo wako kwenye Programu ya Outline ili uunganishe na seva ya Outline.