Skip to main content

Kuunganisha kifaa chako kwenye seva ya Outline

Kuunganisha kifaa chako kwenye seva ya Outline

Ili uunganishe kifaa chako kwenye seva ya Outline, ni lazima msimamizi wa seva akutumie mwaliko wa kuunganisha katika seva yake ukitumia ufunguo wa kipekee. Mwaliko huu:

  • Utakuomba upakue kisha uweke Outline kwenye kifaa chako ikiwa huna
  • Utatumia ufunguo kufanya muunganisho salama kati yako na seva ya Outline

Ukishaunganisha kwenye seva, unaweza kubofya "unganisha" au "tenganisha" ili utumie Outline.

Muhimu: Outline haifanyi kazi bila ufunguo na seva ya Outline. Kupakua na kuweka programu ya Outline kwenye kifaa bila ufunguo hakutalinda shughuli zako kwenye intaneti.