Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kuweka mipangilio ya seva ya Outline
Ninaweza kutumia Outline bila seva?
Hapana. Programu ya Outline inahitaji uwezo wa kufikia seva, iwe inadhibitiwa na shirika lako, mhusika mwingine unayemwamini au unaidhibiti mwenyewe.
Inachukua muda gani kuweka mipangilio ya seva ya Outline?
Katika hali nyingi, chini ya dakika 5. Unaweza kuweka Outline kwenye seva yoyote ya wingu, lakini tulishirikiana na DigitalOcean kukupa hali rahisi kutumia yenye maelekezo ya kuweka, ambapo unaweza kuweka mipangilio ya seva yako kwa hatua chache—hakuna hati.
Ukichagua AWS, GCP au mipangilio ya kina, tumerahisisha mchakato wa kuweka seva katika hati moja inayoshughulikia mazingira mengi.
Ninaweza kuweka wapi mipangilio ya seva ya Outline?
Unaweza kuweka mipangilio ya seva ya Outline kwenye watoa huduma wengi wa wingu popote wanapofanya kazi.
Chaguo rahisi zaidi ni kuiwekea mipangilio kwenye DigitalOcean, kwa kuwa ina seva katika maeneo mengi, kama vile Amsterdam, Toronto, San Francisco na Singapore. Ikiwa unapendelea kuweka kwenye mtoa huduma za wingu mwingine au kwenye miundomsingi yako mwenyewe, unaweza kuchagua ‘Hali ya Kina’ katika programu ya Kidhibiti cha Outline kisha ufuate maagizo ya kuweka ukitumia hati ya kuweka mipangilio.
Ninapaswa kuweka wapi mipangilio ya seva yangu ya Outline?
- Kuna mambo machache ya kuzingatia unapochagua mahali Seva yako ya Outline itakapokuwa:
- Mahali Seva ya Outline ilipo huathiri hali ya utumiaji wa intaneti. Kwa mfano, ikiwa seva inapatikana Amsterdam, mtumiaji anayefikia seva hiyo atapata hali ya utumiaji wa intaneti kana kwamba yuko Uholanzi. Huenda hata baadhi ya tovuti zikaonyeshwa kwa lugha ya Kiholanzi. Kwa kawaida, unaweza kubatilisha lugha ya mahali seva ilipo ukitumia kiteuzi cha lugha kwenye tovuti.
- Umbali kati ya watumiaji wako na Seva ya Outline unaweza kuathiri kasi. Kwa jumla, umbali halisi kati ya watumiaji wa Outline na seva unaweza kuathiri kasi za intaneti ya watumiaji. Katika hali nyingi, unaweza kuchagua eneo la seva lililo karibu zaidi na watumiaji wako watarajiwa, lakini unaweza kuangalia Ramani ya Kebo ya Majini ili uone kebo zipi za intaneti zimeunganishwa kwenye nchi au eneo lako.
- Mahali seva yako ya VPN ilipo panaweza kuathiri mfumo wa kisheria. Tafadhali kumbuka kuwa programu ya Outline haihifadhi kumbukumbu ya trafiki yako. Pata maelezo zaidi kuhusu Usalama na faragha unapotumia Outline.