Jinsi ya kuweka mipangilio ya seva nyingi za Outline
Ili uweke mipangilio ya Seva za ziada za Outline, bofya aikoni ya “+” kwenye kidirisha cha usogezaji kilicho upande wa kushoto wa programu yako ya Kidhibiti cha Outline. Maagizo ya kuongeza seva mpya ni sawa na unayotumia wakati unasakinisha seva yako ya kwanza.
- Hatuna kikomo cha idadi ya seva za Outline unazoweza kuweka.
- Kwa kila seva ya Outline utakayoweka, utahitaji mashine pepe mahususi.
- Hatua ya kuweka mashine pepe za ziada inaweza kuongeza ada zako kutoka kwa huduma ya wingu unayotumia. Tafadhali angalia kifurushi chako cha bei kutoka kwa mtoa huduma za wingu unazotumia ili uhakikishe unafahamu cha kutarajia.
Kuunda seva ya ziada ya Outline kwenye DigitalOcean
Baada ya kubofya aikoni ya + na kuchagua kuweka kwenye DigitalOcean, utafuata maagizo sawa na yale uliyotumia kuweka mipangilio ya seva yako ya kwanza. Aidha, kwa vile Outline Manager huunganika na DigitalOcean, tutaweza kukutengenezea mashine pepe bila wewe kulazimika kuondoka kwenye programu ya Outline Manager.
Kumbuka kwamba Outline Manager inaweza tu kuruhusu akaunti moja ya DigitalOcean kwa wakati mmoja. Ikiwa ungependa kuweka au kuunda seva nyingine za Outline ukitumia akaunti nyingine za DigitalOcean, unaweza kuziweka ziwe na mipangilio ya kina.
Kuweka seva ya ziada ya Outline kwenye GCP, AWS au mtoa huduma mwingine wa seva ya wingu
Anza kwa kuunda mashine pepe mpya ukitumia mtoa huduma za wingu uliyechagua. Kisha, fungua Outline Manager na ukamilishe maagizo ya usakinishaji wa kina kama vile huenda ulifanya mara ya kwanza.