Skip to main content

Mfumo wa Wingu la Google wa Kuweka Mipangilio Kiotomatiki

Muhtasari

Outline Manager ina kipengele kinachokuruhusu kuweka mipangilio kiotomatiki kwenye Outline Server katika seva inayofanya kazi kwenye Google Cloud. Ukichagua kutumia kipengele hiki, Kidhibiti cha Outline kitakuomba uingie ukitumia Akaunti yako ya Google, ambayo itatoa ruhusa fulani zaOAuth kwa Kidhibiti cha Outline ulichoweka kwenye kifaa chako kwa madhumuni ya kuweka mipangilio kwenye Akaunti yako ya Wingu la Google.

Ikiwa hungependa kutoa ruhusa hizi, unaweza kufuata maagizo ya kuweka mipangilio ya kina katika Kidhibiti cha Outline ili utumie Outline kwenye Google Cloud Platform.

Ruhusa Zinazotolewa

Ili iweze kuweka mipangilio kiotomatiki, Outline Manager inahitaji ruhusa zifuatazo kutoka kwa Akaunti yako ya Google.

Google Cloud Platform

  • Kuangalia na kudhibiti nyenzo zako za Google Compute Engine
  • Kuangalia data yako kwenye huduma mbalimbali za Google Cloud na kuona anwani ya barua pepe ya Akaunti yako ya Google

Taarifa za msingi za akaunti

  • Kuangalia anwani ya barua pepe ya Akaunti yako msingi ya Google
  • Kukuhusisha na taarifa zako binafsi kwenye Google

Ruhusa za ziada

  • Kudhibiti miradi yako ya Cloud Platform
  • Kuangalia na kudhibiti akaunti zako za malipo za Google Cloud Platform
  • Kudhibiti mipangilio yako ya huduma ya Google API

Ruhusa hizi hutuwezesha kutumia vipengele vya kiwango cha juu vya kudhibiti seva zako za Outline ikiwa ni pamoja na:

  • Kukuruhusu kuchagua akaunti sahihi ya malipo
  • Kuunda mradi mpya wa kupanga seva zako za Outline
  • Kuorodhesha vituo vya data vinavyopatikana
  • Kuunda kompyuta pepe mpya za kuendesha Outline
  • Kuweka mipangilio ya mashine pepe kwa kutumia Outline

Kubatilisha Ruhusa

Unaweza kubatilisha uwezo wa Outline Manager wa kufikia Google Cloud Platform kwa kutembeleaAkaunti Yangu. Ukibatilisha uwezo wa kufikia, seva zozote ulizounda kwa kutumia mfumo wa kuweka mipangilio kiotomatiki zitaendelea kutumika lakini hazitaonekana katika Outline Manager. Ili urejeshe uwezo wa kuzifikia, unganisha upya kwenye Google Cloud Platform kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka mipangilio kiotomatiki.

Mpangilio wa Mradi wa Outline

Mfumo wa Google Cloud wa kuweka mipangilio kiotomatiki hutumia mradi mmoja waGoogle Cloud project kupanga seva zako za Outline. Mradi huo huundwa mara ya kwanza unapotumia mfumo wa kuweka mipangilio kiotomatiki, ukiwa na kitambulisho cha mradi kinachopendekezwa kinachoanza kwa “Outline-” na kufuatiwa na herufi zingine nasibu. Ukipenda, unaweza kuchagua kitambulisho tofauti cha mradi wakati unaundwa. Mradi utaitwa “Seva za Outline”.

Akaunti ya Bili

Miradi ya Wingu la Google inahitaji uunganishe “akaunti ya malipo” inayobainisha maelezo ya malipo. Unapotumia kwa mara ya kwanza mfumo wa Google Cloud wa kuweka mipangilio kiotomatiki, utaombwa uwe na akaunti ya malipo itakayohusishwa na seva zako za Outline. Wakati mwingine seva itaacha kufanya kazi kwa sababu kuna tatizo la akaunti ya malipo Katika hali hii, unapaswa kuingia katika akaunti kwenyeDashibodi ya Google Cloud, utafute mradi wa Google Cloud unaohusishwa na Outline (unaoitwa “Seva za Outline”), kisha usasishe mipangilio ya malipo.

Kuharibu Seva

Ikiwa ungependa kuharibu seva zako zilizoundwa kwa kutumia mfumo wa kuweka mipangilio kiotomatiki, njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo ni katika Kidhibiti cha Outline. Hata hivyo, ikiwa ungependa kuharibu seva hizo wewe mwenyewe, unaweza kuingia katika akaunti kwenyeDashibodi ya Google Cloud, utafute mradi ulioundwa wakati wa kuweka mipangilio kwa mara ya kwanza (unaoitwa “Seva za Outline”), kisha ufute nyenzo zilizopo au ukomeshe mradi.