Skip to main content

Ninawezaje kufuta seva yangu ya Outline?

Ni rahisi kwa watoa huduma wengi wa wingu kuondoa mashine pepe maalum unayotumia.

Iwapo unatumia DigitalOcean kama mtoa huduma za wingu, unaweza kufuta mashine pepe yako iliyopo kwa kubofya kitufe cha gia na kuchagua "Haribu Seva". Baada ya kufanya hivyo, utaombwa uunde mashine pepe mpya katika mahali utakapochagua.

Ukiondoa seva ya Outline, itafutwa kabisa na funguo zake hazitafanya kazi tena. Iwapo hungependa shughuli za watu za ufikiaji wa Outline zikatizwe, utahitaji kuweka mipangilio ya seva mpya ya Outline kisha uruhusu ufikiaji kabla ya kufuta seva yako ya zamani.